LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wataalam wakutana jijini Dodoma kutafuta mbinu za kuendeleza Kilimo cha Umwagiliaji


Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Washiriki wa mkutano wa kubadilishana mawazo kuhusu mradi wa kujengea uwezo wakulima na wataalam katika masuala ya Kilimo cha Umwagiliaji wakijadili maswala ya utekelezaji wa mradi unaokaribia kufikia ukingoni mwaka huu 2020.
Washiriki wakisikiliza mawasililisho katika mkutano wa wadau wa kubadilishana mawazo ya kitaalam kuhusiana na Mradi wa kuwajengea uwezo wataalam na wakulima katika Kilimo cha Umwagiliaji.
Washiriki wa mkutano huo wakijadiliana kuhusu mafanikio, changamoto na namna ya kutatua changamoto na namna ambavyo mradi huo unaweza kutekelezwa na kuwa endelevu.
Remigius Rushomesa ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu namna ambavyo mradi wa kuwajengea uwezo wakulima na wataalam katika kilimo cha umwagiliaji unavyoweza kuwa endeleevu hata baada ya kuisha muda wake.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wataalam wa kilimo cha umwagiliaji wameendelea na majadiliano jijini Dodoma huku wakibadilishana mawazo na uzoefu kuhusiana na mradi wa kuwajengea uwezo wakulima na wataalam katika Kilimo cha Umwagiliaji.

Pia wataalam hao wamejikita katika shughuli za mradi huo, mafanikio na changamoto na namna ya kutatua changamoto zilizojitokeza ili kuchochea kilimo cha umwagiliaji nchini kuwa endelevu.

Wataalam hao walifanya mawasilisho ya mpango kazi kupitilia utekelezaji wa mradi kama vile kazi za upembuzi yakinifu katika miradi ya kilimo cha umwagiliaji ambayo hufanyika kabla ya mradi kuanza na mradi kutekelezeka jambo ambalo linapelekea ubora na uimara wa miundombinu ya umwagiliaji.

Sambamba na hilo, mawasilisho pia yalilenga katika majadiliano yaliyohusu tathmini na ufuatiliaji katika swala zima la matumizi na matunzo ya miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji hasa katika eneo la matunzo ya miundmbinu hiyo.

Mradi huo ulianza kazi kwa awamu ya kwanza kutoka Disemba 2010 hadi Juni 2014, awamu ya pili kutoka Agosti 2015 hadi Agosti 2019 na kuongezewa muda kuanzia Septemba 2019 hadi Augusti 2020 ambapo mradi huo unaoelekea ukingini mwaka huu unafadhiliwa na Shirika na Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

No comments:

Powered by Blogger.