Mzee Mkapa atambulisha Kitabu chake jijini Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Rais Mstaafu
wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Mzee Benjamin William Mkapa amesema kusudio la
kuandika kitabu cha maisha yake (My Life, My Purpose- Maisha Yangu, Kusudio
Langu) ni kuweka wazi masuala mbalimbali yakiwemo ya uongozi ambayo
hayafahamiki.
Mzee Mkapa
aliyasema hayo Februari 21, 2020 jijini Mwanza wakati akizungumza kwenye
utambulisho wa kitabu hicho na kuongeza kwamba watu wengi hususani wanasiasa
wanamlaumu kwa Sera alizotekeleza ikiwemo ubinafsishaji lakini wakisoma kitabu
cha “My Life, My Purpose” watapata ukweli wa mambo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (kushoto) kitabu cha "My Life, My Purpose".
Viongozi na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya utambulisho wa kitabu cha "My Life, My Purpose" jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> Habari kuhusiana na Mkapa
No comments: