MWANZA "shirika la KIVULINI lasaidia ujenzi wa masoko ya kisasa na ya mfano"
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Baada ya
kufanya utafiti na kubaini wafanyabiashara wadogo wanakabiliwa na mazingira
magumu ya kufanyia shughuli zao, Shirika la kutetea haki za wanawake na
wasichana (KIVULINI) kwa kushirikiana na Shirika la misaada kutoka Uingereza (I4ID)
limeanza ujenzi wa masoko ya kisasa mkoani Mwanza yatakayokuwa mfano pia katika
kuboresha masoko mengine nchini.
Masokoko
hayo yanajengwa katika eneo la Kiloleli Manispaa ya Ilemela pamoja na Mirongo
jijini Mwanza yakihusisha miundombinu bora na rafiki kibiashara ikiwemo vyoo, eneo
maalumu kwa akina mama kunyonyeshea pamoja na Kituo cha daladala Kiloleli.
Soko la
Kiloleli linatarajiwa kugharimu shilingi Milioni 127 huku soko la Mirongo
likigharimu shilingi Milioni 90.8 ambapo ujenzi huo unatarajiwa kukamilika
katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Februari 2020.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> Habari kuhusiana na KIVULINI
No comments: