LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shuhudia ufunguzi wa Shule mpya ya Mwanza Lutheran

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria, Andrew Gulle amefanya ufunguzi rasmi wa Shule mpya ya Mwanza Lutheran Secondary School (MLSS) iliyopo Mtaa wa Majengo Mapya katika Kata ya Mabatini jijini Mwanza.

Ufunguzi huo ulifanyika Februari 18, 2020 ambapo mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (Tazama hapa https://youtu.be/SiOj06cpJ7k) lakini kutokana na mwingiliano wa majukumu alishindwa kufika na hivyo Askofu Gulle kubeba jukumu hilo.

Miundombinu ya Shule hiyo iliyokamilika ni pamoja na vyumba vinne vya madarasa, maabara tatu, maktaba moja, jengo la utawala, vyoo matundu 24, mabafu matatu ambapo ujenzi wa bwalo la chakula na jiko unaendelea. Ujenzi huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 500 hadi sasa.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.