LIVE STREAM ADS

Header Ads

Hospitali ya Rufaa Bugando yatoa elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Kifafa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando yatoa elimu kwa wananchi pamoja na watumishi wa afya kuhusu ugonjwa wa Kifafa ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Kifafa Duniani Februari 10, 2020.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Profesa Abel Makubi amebainisha kwamba hospitali hiyo imenunua kipimo cha kubaini ugonjwa wa Kifafa hivyo wananchi wasiwe na imani potofu kuhusu ugonjwa huo hatua inayosababisha kuwapeleka wagonjwa kwenye tiba za miti shamba.
 Mkuu wa Idara ya Watoto Hospitali ya Rufaa Bugando, Dkt. Neema Kayange akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo.
 Daktari wa Mishipa ya Fahamu (Idara ya Watoto) Hospitali ya Rufaa Bugando, Dkt. Yusuph Jamnagerwalla amesema wananchi pamoja na watumishi wa afya wanaelimishwa kuhusu ugonjwa wa Kifafa ili kuwajengea uwezo wa kutoa huduma ya kwanza kwa mtu anayeugua ugonjwa huo.
Daktari wa Mishipa ya Fahamu (Idara ya Watoto) Hospitali ya Rufaa Bugando, Dkt. Yusuph Jamnagerwalla amebainisha kuwa Kifafa unazuilika hivyo elimu inaendelea kutolewa kwa jamii pamoja na watumishi wa sekta ya afya ili kuhakikisha watoto wanaozaliwa hawapati matatizo wakati wa kuzaliwa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Profesa Abel Makubi akiwaongoza watoto kukata keki kama ishara ya kutowanyanyapaa wenye ugonjwa wa Kifafa.
  Mmmoja wa watoto akimlisha keki Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Profesa Abel Makubi wakati wa maadhimisho hayo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Profesa Abel Makubi akimlisha keki mmoja wa watoto kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Profesa Abel Makubi akimlisha keki mmoja wa watoto kwenye maadhimisho hayo. 
 Zoezi la kuwaelimisha wananchi kuhusu ugonjwa wa Kifafa.
 Watumishi wa afya wakipata elimu kuhusu ugonjwa wa kifafa.
 Hospitali ya Rufaa Bugando inaona wagonjwa kati ya 20 hadi 40 kwa juma moja ambapo kwa mwaka jana ilihudumia wagonjwa wa Kifafa zaidi ya 1,500.
 Wananchi na watumishi wa afya wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Hospitali ya Rufaa Bugando sasa imeanzisha kampeni ya kutokomeza Kifafa Kanda ya Ziwa.
 Wananchi wanahimizwa kuwahi kwenye vipimo wanapoona mgonjwa ana dalili za ugonjwa wa Kifafa badala ya kwenda kwenye tiba za asili.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.