LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mfuko wa WCF watoa mafunzo kwa Madaktari Kanda ya Ziwa “watoe ripoti sahihi”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) watoa mafunzo kwa watoa huduma za afya wakiwemo Madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kuwajengea uwezo wa kufanya tathmini na kutoa ripoti sahihi kwa wafanyakazi wanaoumia kazini.

Mafunzo hayo ya siku tano kuanzia Februari 10, 2020 yamefunguliwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella aliyewasihi washiriki kuzingatia elimu watakayoipata ili kuhakikisha wanasaidia wafanyakazi wanaoumia kazini kupata fidia stahiki.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa wataalam wa afya Kanda ya Ziwa yanayofanyika jijini Mwanza.
 Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
 Wataalamu wa afya Kanda ya Ziwa wakiwemo Madaktari wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kufanya tathmini sahihi kwa wafanyakazi wanaoumia kazini kabla ya kulipwa fidia na mfuko wa WCF.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (wa tatno kushoto), viongozi wa mfuko wa WCF akiwemo Kaimu Mkurugenzi WCF Anselim Peter (wa tano kulia) pamoja na wataalamu wa afya Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.