LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kampuni ya Songoro Marine yaanza ujenzi wa Kivuko kipya cha Serikali ya Uganda

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport ya jijini Mwanza imezidi kutanua wigo wake kimataifa baada ya kushinda zabuni ya kutengeneza Kivuko kipya (Ferry) cha MV. Buvuma kitakachomilikiwa na Serikali ya Uganda.

Hafla ya uwekaji uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Kivuko hicho ilifanyika Februari 08, 2020 jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Viwanda wa Uganda, Agrey Bagiire (kushoto) huku mwenyeki wake akiwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia).

Itakumbukwa kampuni hiyo imejizolea umaarufu mkubwa baada ya kutengeneza na kukarabati vivuko mbalimbali hapa nchini ikiwemo MV. Mwanza huku pia ikishirikiana na kampuni kutoka Korea kwenye uundaji wa meli mpya na ya kisasa ndani ya Ziwa Victoria.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Waziri wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Viwanda wa Uganda, Agrey Bagiire akizungumza kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa Kivuko cha MV. Buvuma cha nchini humo.
 Waziri wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Viwanda wa Uganda, Agrey Bagiire akichomelea moja ya eneo la Kivuko cha MV. Buvuma kama ishara ya kuanza rasmi ujenzi wa Kivuko hicho.
 Waziri wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Viwanda wa Uganda Agrey Bagiire (wa nne kulia), Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (wa tano kushoto), Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro Marine pamoja na viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakiwa kwenye picha ya pamoja.
 Wafanyakazi wa kampuni ya Songoro Marine wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Tanzania na Uganda.
 Wafanyakazi wa kampuni ya Songoro Marine wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Tanzania na Uganda.
 Viongozi wa Tanzania na Uganda wakiwa kwenye picha ya pamoja.
  Viongozi wa Tanzania na Uganda wakiwa kwenye picha ya pamoja.
 Viongozi wa Tanzania na Uganda wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.