LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya FADev yatoa mafunzo kwa Wanahabari Kanda ya Ziwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Matumizi ya kemikali ya Zebaki kwa ajili ya kuchenjulia dhahabu dhahabu yametajwa kuwa kichochea kikubwa cha athari za kiafya katika jamii pamoja na mazingira.

Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Geita, Herman Matemu aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa yaliyoandaliwa na taasisi ya kuendeleza uchimbaji mdogo wa madini (FADev) ili kuwajengea uwezo kuandika habari za kuelimisha wachimbaji wadogo ili kufanya shughuli zao bila madhara.

Mafunzo hayo ya siku tatu kuanzia Februari 11, 2020 yanayofanyika mjini Geita yalishirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga pamoja na Geita.

Mwenyekiti wa taasisi ya FADev, John Bosco alisema Serikali imeweka mazingira mazuri kwa ajili ya wachimbaji wadogo kufanya shughuli zao hivyo ni vyema wakazingatia taratibu za kisheria hususani katika kuendelea sekta hiyo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo waliahidi kuyatumia vyema ili kuelimisha wananchi juu ya shughuli sahihi na salama za uchimbaji madini ikiwemo kuondokana na matumizi ya kemikali ya Zebaki bila kinga kwani ina madhara makubwa kiafya.
#BMGHabari

Mwenyekiti wa taasisi ya FADev (Foundation for ASM Development), John Bosco akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mratibu kutoka taasisi ya kuendeleza uchimbaji mdogo wa madini FADev, Evans Rubara akitoa ufafanuzi kuhumu mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kuandika habari za kuelimisha wachimbaji wadogo ikiwemo uchimbaji salama. Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyowashirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa yalianza Februari 11, 2020 mkoani Geita.

Katibu Tawala Msaidizi (Utawala na Rasilimali Watu) Mkoa Geita, Herman Matemu akizungumza wenye ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel.
Baadhi ya washiriki wakijadiliana jambo wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.