Mwenyekiti MPC aapa kutetea maslahi, ulinzi na usalama wa wanahabari
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti mpya wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (Mwanza Press Club- MPC), Edwin Soko akitoa neno la shukurani baada ya wanachama wa Klabu hiyo kumuamini na kumchagua kwa mara nyingine kushika nafasi hiyo kupitia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Machi 07, 2020 jijini Mwanza. Kulia ni Makamu Mwenyekiti MPC, Alex Mchomvu na kushoto ni Katibu Mkuu MPC, Benard James.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Viongozi wapya MPC wakishikana mikono kama ishara ya umoja na mshikamano.
Viongozi wapya MPC wakinyoosha mikono juu kwa pamoja kama ishara ya umoja na mshikamano katika utendaji wa majukumu yao.
Viongozi wapya wa MPC wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Makamu Mwenyekiti MPC, Alex Mchomvu akitoa neno la shukurani baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Katibu Mkuu MPC, Benard James akitoa neno la shukrani.
Mhazi MPC, Paulina David ambaye pia amechaguliwa kwa mara nyingine kushika nafasi hiyo akitoa neno la shukurani kwa wanachama kumuani na kumchagua tena.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Alphonce Tonny akitoa neno la shukurani.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Wambura Mtani akitoa shukurani zake baada ya uchaguzi huo.
Katibu Mkuu Msaidizi MPC, Blandina Alisteds akitoa neno la shukurani baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Chausiku Said akitoa neno la shukurani.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Kisali Simba akitoa neno la shukurani baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Viongozi wa mpitoa MPC wakiwa wameshikana mikono kama ishara ya umoja na mshikamano wakati wakijiuzulu nafasi zao kabla ya Uchaguzi kufanyika.
Awali Katibu Mkuu MPC aliyemaliza muda wake, Magreth Kusekwa akiomba ridhaa kuendelea kuongoza nafasi hiyo ambapo hata hivyo kura hazikutosha.
Katibu Mkuu Msaidizi MPC aliyemaliza muda wake, Projestus Binamungu akiomba ridhaa kuendelea kuongoza nafasi hiyo ambapo hata hivyo kura hazikutosha.
Awali Mjumbe Kamati Tendaji MPC aliyemaliza muda wake, Nashony Kennedy akiomba ridhaa kuwa Katibu Mkuu ambapo hata hivyo kura hazikutosha.
Awali Mjumbe Kamati Tendaji MPC aliyemaliza muda wake, Gloria Kiwia akiomba ridhaa kuwa Mhazini ambapo hata hivyo kura hazikutosha.
Mjumbe Kamati Tendaji MPC aliyemaliza muda wake, Sitta Tumma akiomba ridhaa ya kuendelea kuitumikia Klabu hiyo ambapo hata hivyo kura hazikutosha.
Mjumbe Kamati Tendaji MPC aliyemaliza muda wake, Philmon Malili akiomba ridhaa kuitumikia nafasi hiyo kwa mara nyingine ambapo hata hivyo kura hazikutosha.
Mgombea nafasi ya Mwenyekiti MPC, Mabere Makubi akiomba ridhaa hiyo kwa wapiga kura ambapo hata hivyo kura hazikutodha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi MPC, Jimmy Luhende ambaye pia ni Mwenyekiti Mstaafu MPC akifafanua jambo kabla zoezi la kupiga kura halijaanza.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa
Habari Mkoa Mwanza (MPC), Edwin Soko ambaye amechaguliwa kwa mara ya pili
kushika nafasi hiyo ameahidi kushirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha
maslahi, ulinzi na usalama wa waandishi wa habari vinalindwa.
Soko aliyasema hayo Machi 07, 2020
kwenye Mkutano Mkuu wa MPC ulioambatana na uchaguzi wa viongozi wapya wa kuiongoza
Klabu hiyo kwa miaka mitano ijayo hadi 2025 kufuatia tamati ya viongozi wa
mpito waliongia madarakani Juni Mosi 2019 kupitia Mkutano Mkuu Maalum.
“Lazima tuhakikishe tunairejesha Klabu
kule ilikotoka na hakika lazima tufanye kazi usiku na mchana ili kulifikia hili
na niwaahidi waandishi wa habari kwamba nitahakikisha tunatetea maslahi yao
pamoja na suala la ulinzi na usalama wao” alisisitiza Soko.
Katika uchaguzi huo, viongozi
waliochaguliwa ni Mwenyekiti Edwin Soko aliyetetea nafasi yake kwa kura 57
dhidi ya tisa za mshindani wake Mabere Makubi, Makamu Mwenyekiti Alex Mchovu aliyepata
kura 42 na kumuondoa kwenye nafasi hiyo Albert Sengo aliyepata kura 23.
Upande wa Katibu Mkuu aliyechaguliwa
ni Benard James aliyepata kura 36 na kumuondoa Magreth Kusekwa aliyepata kura
15. Wengine ambao kura hazikutosha ni aliyekuwa Mjumbe Kamati Tendaji Nashon
Kennedy aliyepata kura sita pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu Msaidizi Projestus
Binamungu aliyepata kura nane huku nafasi ya Katibu Mkuu Msaidizi ikienda kwa mgombea
pekee Blandina Alistides aliyepata kura 52 za ndiyo dhidi ya kura 13 za hapana.
Nafasi ya Mweka Hazina ilibaki kwa
mwenye nayo Paulina David akiyepata ushindi mwembamba wa kura 33 dhidi ya
mpinzani wake Gloria Kiwia ambaye awamu iliyopita alikuwa Mjumbe Kamati Tendaji
aliyepata kura 32 huku Wajumbe watano wa Kamati Tendaji wakiwa ni Kisali Simba
(kura 50), Husna Mlanzi (kura 49), Chausiku Said (kura 39), Wambura Mtani (kura
38) pamoja na Alphonce Tonny (kura 36).
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: