Wanawake Misungwi waitumia vyema mikopo kujikwamua kiuchumi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.co
Wanawake katika Wilaya Misungwi mkoani
Mwanza wametajwa kuitumia vyema mikopo inayotolewa na Halmashauri kujikwamua
kiuchumi huku pia wakiwa warejeshaji wazuri wa mikopo hiyo ikilinganishwa na makundi
mengine.
Hayo yalibainishwa na Mratibu wa
dawati la uwezeshaji wanawake kiuchumi wilayani humo kwenye kongamano la
wanawake ikiwa ni sehemu ya shughuli kuelekea kilele cha siku ya wanawake
duniani ambayo kitaifa mwaka huu 2020 yatafanyika mkoani Simiyu.
Tangu mwaka 2018 hadi Machi 2020 Halmashauri
ya Wilaya Misungwi imetoa shilingi Milioni 298 kama mikopo isiyo na riba kwa
vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa ajili ya kuanzisha
miradi mbalimbali lakini baadhi ya vikundi vinaelezwa kutumia ndivyo sivyo
fedha hizo na hivyo kushindwa kurejesha mkopo.
Kongamano hilo liliandaliwa na shirika
la kutetea haki za wanawake na wasichana KIVULINI huku kauli mbinu ya
maadhimisho ya Siku ya Wanamke Duniani ambayo huadhimishwa Machi 08 kila mwaka
ikiwa ni “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Sasa nay a Baadaye”.
#BMGHabari
Mkurugenzi Mtendaji wa KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye kongamano hilo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Mwanza, Isack Ndasa akizungumza kwenye kongamano hilo ambapo alitoa rai kwa vikundi vinavonufaika na mikopo ya Halmashauri kuitumia vyema mikopo hiyo na kuirejesha kwa wakati badala ya kuitumia kwa anasa.
Baadhi ya wanawake wilayani Misungwi waliohudhuria kongamano hilo.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> Habari zaidi kutoka Misungwi
No comments: