LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wizara nne zaunda Kamati kufanikisha ndoto ya Mzee wa miaka 60 kuwa Bilionea

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com


Mwandishi Wetu, Dodoma
Timu ya wataalam he 9 kutoka Wizara ya Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Viwanda na Biashara na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeundwa ili kumsaidia Mjasiliamali wa miaka 60 kutoka mkoani Njombe wilaya ya Ludewa, Reuben Mtitu maarufu Mzee Kisangani ili kutimiza ndoto yake ya kuwa bilionea baada ya kubuni kiwanda kinachotengeneza zana zinazotokana na madini ya chuma.

Kamati hiyo imeundwa Machi 30, 2020 na Mawaziri Wanne wa Wizara ya Madini Doto Biteko, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mussa Zungu, OR-TAMISEMI Naibu Waziri Mwita Waitara na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi, Stella Manyanya, katika kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano wizara ya madini jijini Dodoma. Wengine waliohudhuria ni kutoka Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Mazingira (NEMC) na Wataalam kutoka wizara ya Madini na Tume ya Madini.

Akifungua kikao hicho, Waziri Biteko aliwaeleza wajumbe hao, kuwa lengo ni kujadili namna ya kumsaidia Mzee Kisangani kwenye kila hatua kutoka mahali alipo ili ikibidi awe bilionea. Ameongeza kuwa, Mzee Kisangani hajui kusoma wala kuandika lakini ameonyesha kitu ambacho kama Serikali inahitaji kumsaidia kwa kila hatua anayohitaji.

Biteko alisema, alipokuwa ziarani mkoani Njombe kuanzia Machi 13-16, 2020 alitembelea kiwanda chake ambapo kwa namna kilivyo, lakini kinatengeneza zana mbalimbali za madini ya Chuma kama vile, Mapanga, Fyekeo, Visu, Majembe huku akiwa amewaajiri watu 30, kutokana na uthubutu na juhudi alizonazo. Waziri Biteko akiwa ziarani katika eneo hilo aliahidi kukutana na Mawaziri wote wanao husiana na shughuli zake ili kujadili namna ya kumsaidia.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mussa Zungu, akichangia namna ya kumsaidia, alisema wizara yake kupitia (NEMC) itahitaji andiko (Bussines Plan) na kwamba wataalam wa eneo hilo watasimama ipasavyo kusaidia Mzee Kisangani kufikia ndoto yake. Wakati Zungu akihitaji andiko, Biteko amesema tayari Chuo Kikuu cha Mzumbe walishajitolea kumuandikia andiko la biashara (Business Plan) ya kiwanda chake.

Naye Naibu Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara, alisema kila mkoa ulipewa agizo la kuandaa maeneo ya uwekezaji hivyo Mkuu wa Mkoa mkoani humo atatoa eneo maalum kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha Kisangani kwenye eneo lililotengwa.

Kwa upande wake, Naibu wa Viwanda na Biashara Mhandisi, Stella Manyanya alisema kumekuwa na changamoto nyingi za kuwasaidia watu wenye ubunifu hususani kutokana na vipengele vilivyowekwa kisheria suala ambalo huwakatisha tamaa. Amesema wizara yake kupitia NDC, SIDO na TIRDO kila taasisi itatoa mtaalam kwa ajili ya kumsaidia mjasiliamali huyu ili afikie malengo.

Mkurugenzi Mkuu wa NDC, Prof. Damian Gabagambi alisema mara baada ya kusoma taarifa za ziara ya waziri wa Madini kupitia vyombo vya habari alituma wataalam kwenda kiwandani hapo na kuona namna gani ya kumsaidia ili kuzalisha chuma na kuongeza uwezo wa uzalishaji.

Waziri Biteko ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, alisema kwakuwa tunataka kuona matokeo ya huyu Mzee kutokana na nguvu za serikali ndipo iliamriwa kuundwa kwa wajumbe wa kamati ya wataalam wa aina mbalimbali ambao ni wizara/taasisi kwenye mabano, Wilfred Machumu (Tume ya Madini), Issa Mtuwa (Wizara ya Madini), Abbas Mruma (GST), Prof. Silvester Mpanduji (SIDO), Prof. Madundo Mtambo Mkumbukwa (TIRDO), Dr. Yohana Mtoni (NDC), Anorld Mapinduzi (NEMC), Leo Mavuka (TAMISEMI), na Dr. Hellen (Chuo Kikuu Mzumbe.

No comments:

Powered by Blogger.