LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kupambana na Corona “marufuku kurandaranda Mwanza”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amezuia watoto kuranda randa ovyo mitaani hususani kipindi hiki Shule zimefungwa ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupambana na maambukizi dhidi ya ugonjwa wa Corona (Covid- 19).

Mongella ameyasema hayo Aprili 01, 2020 wakati wa zoezi la kutoa elimu ya kupambana na Corona kwa watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa Mwanza. Zoezi hilo litalekezwa katika Wilaya zote za Mkoa Mwanza kwa kushirikiana na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Redcross) ambalo limepewa jukumu la kusambaza vipeperushi vya elimu ya kupamba na Corona.

Baada ya kuzungumza na watumishi hao, Mongella akiwa ameambatana na timu ya wataalamu mbalimbali wakiwemo wa afya alitembelea pia maeneo ya umma ikiwemo eneo la feri ya Kigongo-Busisi ili kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Corona ikiwemo kutakasa ama kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Abiria katika kivuko cha Kigongo-Busisi mkoani Mwanza wakinawa mikono kwa maji tiririka kabla ya kuingia kwenye feria.
 Abiria wakinawa mikono kabla ya kuingia kwenye feri kwenye kivuko cha Kigongo-Busisi mkoani Mwanza,
 Feri ya MV. Mwanza inayofanya safari zake kati ya Kigongo wilayani Misungwi na Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akipokea vipeperushi vyenye mwongozo wa kupambana na maambukizi ya Corona kutoka kwa Mratibu wa Redcross Mkoa Mwanza, Salome Tuppa (kushoto).
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akigawa vipeperushi vyenye mwongozo wa kupambana na Corona kwa Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa Mwanza. Vipeperushi hivyo vimetolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kusambazwa na Redcross.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.