RC Mongella azindua zoezi la kutoa elimu ya kujikinga na Corona
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa
Mwanza, John Mongella amezindua rasmi zoezi la kutoa elimu na kusambaza vipeperushi vyenye ujumbe
wa namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid- 19) katika
maeneo mbalimbali ya umma ikiwemo masoko na vituo vya usafiri.
Zoezi hilo linalotekelezwa
na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (RED CROSS) kwa kushirikiana na Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Uzinduzi
huo umefanyika Aprili 01, 2020 ukiambatana na utoaji elimu ya kujikinga na
Corona kwa watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa Mwanza.
Katika
kuhakikisha afua za kupambana na Corona zinatekelezwa, Mongella amekagua
utayari wa kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo katika maeneo yenye
mikusanyiko ya watu ikiwemo kivuko cha Kigongo-Busisi, stendi ya mabasi Nyabulogoya,
soko la Mirongo na Mbugani ambapo amewahimiza wananchi kuzingatia tahadhari
zinazotolewa na Serikali ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka
na sabuni.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza na watumishi wa sekretarieti ya Mkoa Mwanza kabla ya kuzindua zoezi la usambazaji vipeperushi vyenye ujumbe wa kujikinga na Corona.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akipokea kipeperushi kutoka kwa Mratibu wa RED CROSS Mkoa Mwanza, Salome Tuppa (kushoto).
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akipokea bango lenye ujumbe wa namna ya kujikinga na Corona kutoka kwa Mratibu wa RED CROSS Mkoa Mwanza, Salome Tuppa ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa zoezi la kusambaza mabango na vipeperushi hivyo kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akigawa kipeperushi chenye ujumbe wa namna ya kujikinga na Corona.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akigawa kipeperushi chenye ujumbe wa namna ya kujikinga na Corona kwa watumishi wa sekretarieti ya Mkoa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akigawa kipeperushi chenye ujumbe wa namna ya kujikinga na Corona.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: