LIVE STREAM ADS

Header Ads

Juhudi za kupambana na Corona zashika kasi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Tahadhari mbalimbali ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka zinaendelea kuchukuliwa katika maeneo yenye mikusanyiko wa watu ikiwa ni sehemu ya kupambana na maambukizi ya Corona ambapo pichani ni moja ya eneo la kunawia mikono katika stendi ya mabasi Nyabulogoya jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa tatu kushoto) akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali kukagua utayari wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Corona katika vituo vya usafiri na masoko.
Wananchi wanasisitizwa kuzingatia ushauri wa kiafya unaotolewa ili kuepuka maambukizi ya Corona.
Afua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa na wananchi katika mikoa mbalimbali Tanzania ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni ili kudhibiti kusambaa maambukizi ya virusi vya Corona (Covid- 19).

Wazazi na walezi nao wanakumbushwa kutowaacha watoto wao kuzurura ovyo mitaani katika kipindi hiki ambacho shule zimefungwa huku wanandoa wakihimizwa kuimarisha mahusiano yao zaidi katika kipindi hiki ambacho wanapata muda mwingi wa kuwa pamoja nyumbani tofauti na hapo awali kabla ya janga la Corona.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.