LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA “shirika la KIVULINI lakabidhi vifaa kwa wanahabari”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI Mei 19, 2020 limekabidhi msaada wa vifaa vya kujikinga na mambukizi ya virusi vya Corona (Covid- 19) kwa waandishi wa habari mkoani Mwanza.

Mkurugenzi wa shirika hilo, Yassin Ally amesema vifaa hivyo vitawasaidia waandishi wa habari ambao ni kundi muhimu katika mapambano dhidi ya Corona kutimiza vyema majukumu yao hususani kuwaelimisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi hayo.

Wakipokea vifaa hivyo ikiwemo ndoo za lita 20, matenki ya lita elfu moja, vitakasa mikono pamoja na mashine za kupimia joto la mwili (Thermometer), baadhi ya waandishi wa habari walitoa rai kwa wadau wengine kuendelea kuwaunga mkono kwani wamekuwa wakisahaulika pale vifaa vya kujikinga na Corona vinapotolewa kwa makundi mengine.

Mbali na waandishi wa habari, shirika la KIVULINI limeanza kukabidhi vifaa kama hivyo kwa wanaharakati wa kujitolea ngazi ya jamii katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na Kigoma vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya shilingi milioni 15.
#BMGHabari
Afisa wa shirika la KIVULINI, Yunis Mayengela (kulia) akikabidhi barakoa kwa mwandishi wa TBC, Michael Obunde (kushoto) kwa ajili ya kuzigawa kwa waandishi wa habari mkoani Mwanza.
Afisa wa shirika la KIVULINI, Yunis Mayengela (kulia) akikabidhi kifaa cha kupimia joto la mwili kwa mwandishi wa TBC, Michael Obunde (kushoto) kwa ajili ya kuwahudumia waandishi wa habari mkoani Mwanza.
Afisa wa shirika la KIVULINI, Yunis Mayengela (kulia) akimpima joto la mwili mwandishi wa TBC, Michael Obunde (kushoto).
Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kushoto) akikabidhi ndoo na kitakasa mikono kwa mwanablogu wa BMG, George Binagi (kulia).
Afisa wa shirika la KIVULINI (kushoto) akikabidhi tenki la maji kwa wawakilishi wa Sahara Media Group.
Afisa wa shirika la KIVULINI (kushoto) akikabidhi tenki la maji kwa wawakilishi wa TBC.
Vifaa mbalimbali ikiwemo ndoo kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya Corona.
Waandishi wa habari zaidi ya 30 mkoani Mwanza wamenufaika na vifaa hivyo.
Waandishi wa habari mkoani Mwanza wakiwa na ndoo za kunawia maji.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Mwanza walionufaika na msaada huo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.