LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shehena ya samaki yasafirishwa kimataifa kutokea uwanja wa ndege wa Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo la mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwanza, kwa mara ya kwanza shehena ya minofu ya samaki kiasi cha tani nane imesafirishwa moja kwa moja kutoka katika uwanja huo kuelekea Bara Ulaya katika mji wa Brussels nchini Ubelgiji.

Kuanza kwa safari za ndege za kimataifa Mei 12, 2020 kumeshuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega pamoja na Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (wa pili kushoto) akikagua boksi la minofu ya samaki kabla ya kuingizwa kwenye ndege kwa ajili ya kusafirishwa moja kwa moja kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza kwenda Brussels nchini Ubelgiji.
 Sehemu ya minofu hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya Tanzania Fish Processors ikibebwa kwa ajili ya kuingizwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Rwanda kwa ajili ya kusafirishwa moja kwa moja kwenda Brussels nchini Ubelgiji.
 Viongozi mbalimbali waliojitokeza kushuhudia usafirishaji wa minofu ya samaki yenye uzito wa tani nane kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza moja kwa moja kwenda Brussels Ubelgiji wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.