DC Misungwi akagua uzalishaji wa viwanda 'ahimiza kazi iendelee'
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, Juma Sweda Jumatano Mei 13, 2020 akikagua uzalishaji wa viwanda mbalimbali wilayani humo na kuhimiza wawekezaji wenye viwanda kuendelea na uzalishaji.
#BMGHabari
Wafanyakazi katika kiwanda cha Sayona Steel kilichopo eneo la Nyang'homango wakiendelea na uzalishaji wa sufuria.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Mkuu wa kiwanda cha Sayona Steel, Sunny Naker kuhusu uzalishaji wa sufuria.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda akikagua uzalishaji wa nondo katika kiwanda cha Sayona Steel.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda pia alikagua ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza mikate cha Royal Bakery kinachojengwa Nyashishi wilayani Misungwi.
Mwakilishi wa kiwanda cha kutengeneza mikate cha Royal Bakery, Yusuph Daud (wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda aliyeambatana na viongozi mbalimbali kwenye ziara ya kutembelea kiwanda hicho.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> Habari kutoka Misungwi
No comments: