LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya TAHA yawasaidia wakulima Mwanza kuzalisha kwa tija

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Vijana wanaojishughulisha na kilimo cha mboga mboga na matunda jijini Mwanza wameishukuru taasisi ya TAHA (Tanzania Horticultural Association) kwa kuwajengea uwezo na hivyo kuzalisha mavuno yenye ubora.

Wakizungumza Juni 15, 2020 kwenye zoezi la uvunaji wa zao la pilipili hoho, vijana wa kikundi cha Young Adult kilichopo Malimbe jijini Mwanza walisema TAHA imewajengea utaalam na mbinu za kilimo cha kisasa na hivyo kuzalisha kwa tija.

"Tulizoea kulima kilimo cha kawaida bila kujali utaalam ambao ungetuwezesha kupata mazao zaidi. Lakini tulipojiunga na TAHA wametusaidia namna ya kuandaa na kulihudumia shamba vizuri pamoja na umwagiliaji kwa njia ya matone" alisema Kulwa Magembe ambaye ni Mwenyekiti wa kikundi cha Young Adul kilichopo Malimbe jijini Mwanza.

Naye Mwenyekiti wa kikundi cha vijana Nyakalekwa kilichopo Luchelele jijini Mwanza, Samwel Luchagula alisema taasisi ya TAHA imewasaidia kujiamini na kuendeleza miradi ya kilimo na hivyo kujitegemea kiuchumi badala ya kuishi kwa utegemezi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa kikundi cha Young Adult, Kulwa Magembe akishiriki uvunaji wa zao la pilipihi hoho kwenye shamba darasa la kikundi hicho lililopo Malimbe jijini Mwanza.
 Mavuno ya zao la pilipili hoho yakiendelea katika shamba la kikundi cha Young Adult lililopo Malimbe jijini Mwanza.
Wanachama wa kikundi cha vijana cha Young Adult kilichopo Malimbe jijini Mwanza wakivuna zao la pilipili hoho. 
Mavuno ya pilipili hoho yakiendelea katika shamba darasa la kikundi cha Young Adult kilichopo Malimbe jijini Mwanza.
Mtaalam wa kilimo cha mboga mboga na matunda kutoka Taasisi ya TAHA, Brison Sabuni (kulia) akishiriki kwenye mavuno ya zao la pilipili hoho katika shamba darasa la kikundi cha Young Adult lililopo Malimbe jijini Mwanza.
 Mtaalam wa kilimo cha mboga mboga na matunda kutoka Taasisi ya TAHA, Brison Sabuni (kulia) akishiriki mavuno ya zao la pilipili hoho katika shamba darasa la kikundi cha Young Adult. Kushoto ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Kulwa Magembe.
Mtaalam wa kilimo cha mboga mboga na matunda kutoka Taasisi ya TAHA, Brison Sabuni (kulia) akishiriki kwenye mavuno ya zao la pilipili hoho katika shamba darasa la kikundi cha Young Adult. Kushoto ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Kulwa Magembe. 
 Mavuno ya zao la pilipili hoho yakiendelea katika shamba darasa la kikundi cha Young Adult lililopo Malimbe jijini Mwanza.
 Taasisi ya TAHA imevijengea uwezo vikundi mbalimbali ikiwemo kikundi cha Young Adult ili kuzalisha kwa tija mazao ya mboga mboga na matunda huku ikiwaunganisha pia na masoko.
 Mtaalam wa kilimo cha mboga mboga na matunda kutoka Taasisi ya TAHA, Brison Sabuni akikagua ubora wa matunda ya pilipili hoho katika shamba la kikundi cha Young Adult kilichopo Malimbe jijini Mwanza.
Mwanachama wa kikundi cha vijana Nyakalekwa, Rehema Masasila akishiriki mavuno ya zao la pilipili hoho katika shamba darasa la kikundi hicho lililopo Luchelele jijini Mwanza.
 Mwanachama wa kikundi cha vijana Nyakalekwa, Rehema Masasila anasema taasisi ya TAHA imewasaidia kupata mavuno bora baada ya kuwajengea uwezo.
Mwenyekiti wa kikundi cha vijana Nyakalekwa kilichopo Luchelele jijini Mwanza, Samwel Luchagula akishiriki mavuno ya zao la pilipili hoho kwenye shamba la kikundi hicho.
Mtaalam wa kilimo cha mboga mboga na matunda kutoka Taasisi ya TAHA, Brison Sabuni (kushoto) akishiriki mavuno ya zao la pilipili hoho katika shamba darasa la kikundi cha vijana Nyakalekwa lililopo Luchelele jijini Mwanza. 
Mavuno ya pilipili hoho yakiendelea katika shamba darasa la kikundi cha vijana Nyakalekwa lililopo Luchelele jijini Mwanza.
Mtaalam wa kilimo cha mboga mboga na matunda kutoka Taasisi ya TAHA, Brison Sabuni (kushoto) akitoa ufafanuzi wa namna bora ya kuvuna zao la pilipili hoho katika shamba darasa la kikundi cha vijana Nyakalekwa lililopo Luchelele jijini Mwanza.
Mavuno yakiendelea katika shamba la kikundi cha vijana Nyakalekwa lililopo Luchelele jijini Mwanza. 
Mavuno ya zao la pilipili hoho kutoka shamba la vijana Nyakalekwa lililopo Malimbe jijini Mwanza. 
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.