LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wachimbaji Madini wafariki baada ya kuangukiwa na kifusi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Wachimbaji wawili wa madini wamefariki dunia huku wengine wanane wakijeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi katika mgodi wa wachimbaji wadogo wa dhahabu wa Irasanilo uliopo Kijiji cha Magunga Kata ya Buhemba, Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Juni 12, 2020 kwa kuhusisha maduara mawili ambayo ni namba 139 na 140 ambapo waliofariki ni Kisambi Daud (30) mkazi wa Butiama pamoja na Marwa Mwita (48) mkazi wa Bunda huku majeruhi wakiendelea na matibabu wilayani Butiama.

Hata hivyo kabla ya kutokea kwa tukio hilo, Serikali kupitia kwa Mkaguzi Mkuu wa Migodi, Abdulrahman Mwanga alikuwa ameyafunga maduara yaliyosababisha tukio hilo baada ya kuonekana hatari kiusalama lakini wachimbaji hao waliingia kinyemera usiku.

Waziri wa Madini Doto Biteko amefika katika mgodi huo na kupiga marufuku shughuli za uchimbaji dhahabu kufanyika nyakati za usiku.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini mgodini hapo.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.