LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko aingilia kati mgogoro wa wachimbaji Buhemba “mnampiga askari”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Waziri wa Madini, Doto Biteko amewaagiza viongozi wa Serikali na uongozi wa mgodi wa Irasanilo uliopo Butiama mkoani Mara kukutana na kutafuta suluhisho la mgogoro wa umiliki wa ardhi ulioibuka miongoni mwa wachimbaji wadogo wa dhahabu katika mgodi huo.

Waziri Biteko alitoa maelekezo hayo Ijumaa Juni 12, 2020 alipofika katika mgodi huo kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero zinazowakabili wachimbaji wadogo ambapo alishauri Jumatatu Juni 15, 2020 Mkuu wa Wilaya Butiama pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo kuzikutanisha pande zote zinazong'ang'ania umiliki wa ardhi kwenye baadhi ya maduara ya mgodi huo na kutoa maamuzi kwa kuzingatia haki.

Aidha Waziri Biteko alipiga marufuku shughuli za uchimbaji dhahabu kufanyika nyakati za usiku katika mgodi huo kufuatia wachimbaji wawili kufariki dunia huku wengine wanane wakijeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakifanya shughuli za uchimbaji usiku wa Juni 11, 2020 kwenye maduara mawili ambayo tayari yalikuwa yamefungwa kutokana na usalama mdogo huku akikasirishwa na hatua ya wachimbaji kumpiga jiwe askari wakati anajaribu kuwazuia wasiingie kwenye mashimo hayo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Wachimbaji wadogo katika mgodi wa Irasanilo.
 Viongozi na wachimbaji madini wa mgodi wa Irasanilo.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.