LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko awatoa hofu wachimbaji madini ya viwandani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Waziri wa Madini, Doto Biteko amewatoa hofu wachimbaji wa madini ya viwandani na kuwataka kuwa watulivu wakati Serikali inaandaa utaratibu wa kuwaruhusu usafirishaji wa madini hayo nje ya nchi ambako inaelezwa kuna soko la uhakika.

Waziri Biteko alitoa kauli hiyo Julai 03, 2020 alipotembelea mgodi wa madini ya Manganizi yanayotumika kwenye uzalishaji wa bidhaa za chuma viwandani uliopo Kijiji cha Magamba Kata ya Murusagamba katika Wilaya Ngara mkoani Kagera.

Katika kuhakikisha taratibu za kusafirisha madini hayo zinakamilika kwa wakati, Waziri Biteko aliwaagiza Maafisa Madini nchini hadi kufikia Julai 15, 2020 wawe wamefanya sensa katika migodi yote ya madini ya viwandani ili kubaini aina ya madini na kiasi kinachosubiri kusafirishwa nje ya nchi ili taratibu za kuyasafirisha zifanyike mapema.


Kauli hiyo ya Waziri Biteko ilipokelewa kwa shangwe na Mkurugenzi wa mgodi wa Manganizi Magamba, Sarah Lusambagula aliyesema hatua ya Serikali kuruhusu madini hayo kusafirishwa nje ya nchi itafungua fursa zaidi kibiashara kwa wachimbaji.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa tatu) alimpongeza Mkurugenzi wa mgodi wa Manganizi Magamba, Sarah Lusambagula (wa kwanza) kwa jitihada zake za kusimamia vyema mgodi huo na kuongeza kuwa Wizara itampa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha anafikia mafanikio.
Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Manganizi Magamba wakiwa wamesimama juu ya madini hayo ambayo bado ni ghafi wakati wa ziara ya Waziri wa Madini, Doto Biteko kutembelea mgodi huo.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.