Biteko achachamaa ‘mgodi wa Mwadui kuuzwa kinyemela’
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa
Madini, Doto Biteko ameutaka uongozi wa mgodi wa almasi wa Mwadui (Williamson
Diamond Ltd) hadi kufikia Ijumaa Julai 10, 2020 uwe umewasilisha taratibu
zilizofuatwa kabla ya kutangaza kuuza mgodi huo bila kuishirikisha Serikali
ambayo ina ubia wa asilimia 25.
Biteko
ametoa agizo hilo Jumapili Julai 05, 2020 wakati akizungumza na Menejimenti ya
mgodi huo uliopo Maganzo Wilaya Kishap mkoani Shinyanga huku akieleza kusikitishwa na taarifa ya mgodi huo kuuzwa aliyoipata
kupitia tangazo lililotolewa mtandaoni bila kuishirikisha Serikali.
Mbali na
kuomba taarifa kuhusiana na mgodi huo kuuzwa, Biteko pia ametaka kupewa
taratibu za kikazi zilizofuatwa kabla ya kuwasimamisha baadhi ya wafanyakazi
wake kwa kigezo cha kusitisha uzalishaji ili kufanya matengenezo ya moja ya mitambo
wa kuchenjua almasi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini
No comments: