Kalemani awasweka ndani viongozi wa JUMEME
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani amepiga marufuku makampuni ya kusambaza umeme kwa
kutumia nishati mbalimbali ikiwemo jua, kuwatoza wananchi gharama kubwa
inayozidi shilingi 100 kwa ankra moja.
Dkt.
Kalemani alitoa marufuku hiyo Julai 07, 2020 wakati akizungumza na wananchi katika
Wilaya Sengerema mkoani Mwanza, alipokuwa na ziara ya kukagua utekelezaji wa
miundombinu mbalimbali ya kusambaza
umeme wilayani humo.
Awali Dkt.
Kalemani alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakiilalamikia kampuni ya
JUMEME inayosambaza umeme kwa kutumia nishati ya jua kwa kuwatoza shilingi 3,500
kwa ankra moja ambapo aliamuru viongozi wa kampuni hiyo kukamatwa ili wahojiwe
ni kwa nini wanatoza gharama kubwa kinyume na sheria.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini
SOMA>>> Mchaka mchaka wa Waziri Kalemani
No comments: