Ihefu FC yapeleka kilio Mbao FC
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Timu ya soka ya Mbao FC ya jijini Mwanza imeyaaga mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya ushindi wa nyumbani wa magoli 4-2 dhidi ya Ihefu FC ya jijini Mbeya kwenye mchezo wa 'Play Off''.
Hatua hiyo inatokana na kupoteza mchezo wa kwanza ugenini kwa kichapo cha goli 2-0 na hivyo kufanya matokeo kuwa goli 4-4 ambapo Ihefu imepanda Ligi Kuu kwa faida ya goli la ugenini. Mbao imeungana na Alliance (ya Mwanza pia) katika kuiaga michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Sikiliza Uhuru FM kupitia BMG hapa chini
SOMA>>> Habari mbalimbali za Soka
No comments: