LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wasimamizi watakiwa kutenda Haki Uchaguzi Mkuu 2020

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Kamishna wa Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amewataka viongozi waliokasimiwa kusimamia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, kutimiza vyema wajibu wao kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Nchi. 

Jaji Mstaafu Mihayo ameyasema hayo Agosti Mosi 2020 wakati akifungua mafunzo kwa Waratibu wa Uchaguzi wa mikoa, Wasimamizi na Wasaidizi wa Uchaguzi, Maafisa Uchaguzi na Maafisa Ugavi kutoka mikoa ya Mwanza na Mara. 
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Washiriki wa mafunzo hayo wakila kiapo cha uadilifu/ uaminifu na kujivua uanachama wa vyama vya siasa ili kutenda Haki katika Uchaguzi Mkuu 2020.
 Mratibu wa Uchaguzi Mkoa Mwanza, Mathia Levi akila kiapo cha uadililifu kwenye mafunzo hayo.
 Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya Misungwi, Kisena Mabuba akila kiapo cha uadilifu ili kutimiza wajibu wake kwa haki.
 Msimamizi wa Uchaguzi Musoma Mjini akitoa akitoa shukurani baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo ambapo amesema washiriki wote watanzingatia elimu watakayoipata ili kutimiza vyema wajibu wao kwenye Uchaguzi Mkuu 2020.
Wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu wametakiwa kuyabaini maeneo yao kabla ya uchaguzi ili kutambua ikiwa kuna changamoto ili zitafutiwe ufumbuzi mapema.
 Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania unatarajiwa kufanyika Jumatano Oktoba 28, 2020.
Mafunzo hayo yanafanyika jijini Mwanza kuanzia tarehe 1-3 Agosti 2020.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.