LIVE STREAM ADS

Header Ads

Zoezi la kunyunyizia dawa ya Ukoko kuanza Ukerewe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ameshauri zoezi la kunyunyizia dawa ya ukoko majumbani katika Wilaya ya Ukerewe, kuwafikia wananchi wote hatua ambayo itakasaidia mapambano dhidi ya Malaria.

Mongella ameyasema hayo Agosti 18, 2020 jijini Mwanza wakati akifungua kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya utekelezaji ya unyunyiziaji dawa ya ukoko awamu ya pili wilayani Ukerewe.

Awali Dkt. Laurell Mushi ambaye ni Mratibu wa taasisi ya ABT Associates Mkoa Mwanza alisema awamu ya kwanza ya unyunyiziaji dawa ya ukoko wilayani Ukerewe lililoanza Machi 03, 2020 lililifanikiwa kwa asilimia 92.3 kabla ya kusimama Machi 19, 2020 kutokana na changamoto ya Corona.

Zoezi la unyunyiziaji dawa ya ukoko majumbani wilayani Ukerewe linaratibiwa na taasisi ya “ABT Associates” kupitia ufadhili wa wadau mbalimbali ikiwemo US Aid, CDC, mfuko wa kupambana na Malaria wa Rais wa Marekani pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto (Tanzania).
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.