LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi wachangishana kujenga nyumba za bati

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amezindua kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha jamii kujenga nyumba bora.

Uzinduzi wa kampeni hiyo ulifanyika Agosti 21, 2020 katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ambayo imekuwa wilaya ya mfano nchini kwa kuhamasisha wananchi kujenga nyumba bora kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wakazi wa Misungwi walianza kuhamasishana kujenga nyumba bora za bati na kuachana na nyumba za nyasi baada ya kujengewa uwezo na mashirika mbalimbali ikiwemo shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI.
Kikundi cha Witogwa kinachoundwa na akina mama katika Kata ya Mondo kilianza kuchangiana vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kujenga nyumba bora za bati.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu
Nyumba ya mmoja wa wanachama wa kikundi cha Witogwa.
Wanananchi wilayani Misungwi kupitia vikundi vyao ikiwemo Witogwa wanachangiana vifaa vya ujenzi ili kujenga nyumba za bati na kuondokana na nyumba za nyasi.
Uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya ujenzi wa nyumba bora ulifanyika katika Kata ya Koromije wilayani Misunwgi.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.