Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU Tanzania, Leticia Morice (kulia) akimkabidhi mashine ya kuchakata bidhaa za ngozi Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Rorya mkoani Mara, Charles Chacha kwa ajili ya kuikabidhi kwa kikundi cha WAVIU kiitwacho Nia Moja.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU Tanzania, Leticia Morice akizungumza na wanakikundi wa Nia Moja.
Na Tonny Alphonce, RoryaMwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU Tanzania, Leticia Morice amekabidhi
mashine ya kuchakata bidhaa za ngozi kama vile viatu, mikanda na mabegi kwa kikundi
cha WAVIU cha Nia Moja kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara.
Mashine hiyo
imetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU, Deogratius Rutatwa baada ya kuona jitihada za kujikwamua kiuchumi zinazofanywa
na kikundi cha Nia Moja.
Kikundi cha
Nia Moja ni kati ya vikundi vinavyoundwa na Konga Halmashauri ya Wilaya ya Rorya
ambapo kinaendesha shughuli mbalimbali ikiwemo utengenezaji na ushonaji wa bidhaa za
ngozi, sabuni na mafuta ya kupaka pamoja na kuuza dagaa
waliokaushwa.
Ahadi ya
kukabidhi mashine hiyo ilitimizwa baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU Tanzania, Leticia Morice kukabidhi mashine hiyo yenye dhamani ya shilingi milioni mbili na laki tano mbele uongozi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Rorya, Charles Chacha alilipongeza
Baraza kwa jitihada kubwa zinazofanywa kuviwezesha vikundi ili viweze kujikwamua
kiuchumi huku akiahidi kukipatia kikundi cha Nia Moja kiasi cha shilingi milioni tatu
na laki tano kupitia fedha za mikopo zinazotolewa na Halmashauri kwa makundi
maalum.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Konga ya Rorya, Richard Oloo pamoja na wanakikundi
cha Nia Moja walitoa shukrani za pekee kwa uongozi wa Baraza hilo kupitia Afisa Mtendaji Mkuu wake kwa kuendelea kuwaamini na kuboresha shughuli zao za
kujikwamua kiuchumi na kuahidi kutumia mashine hiyo kuzalisha zaidi na kukuza
mtaji wao.
Habari zaidi kuhusiana na WAVIU
No comments: