LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mgombea CUF aahidi neema kwa wananchi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Ismail Luhamba, Singida
Mgombea wa nafasi ya ubunge Jimbo la Singida Kaskazini mkoani Singida, Mwl. Delphina Frank kupitia Chama cha Wananchi (CUF) amesema akipata ridhaa atahakikisha anaimarisha sekta ya Afya, elimu, maji na nishati jimboni humo.

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kinyagigi kwenye mwendelezo wa kampeni zake za kunadi sera za chama hicho,mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida kaskazini Mwl Delphina Frank ametaja vipaumbele vinne ambavyo atavitekeleza endapo atachaguliwa kuwa Mbunge.

“Wananchi mnaonisikiliza hapa napenda kuwaambia kwamba nina mambo makubwa manne ya kuwafanyia nyinyi katika kipindi cha miaka 5, endapo mtanipa ridhaa ya kuwaongoza nitaanza na Sekta ya Afya, Elimu, Mifugo na Maji.” alisema Delphina.

Mwl Delphina akizungumzia suala la Afya amesema atahakikisha kila Zahanati iliyojengwa na Serikali inakuwa na vifaa tofauti na sasa,kwani kwa sasa kuna majengo tu huku kukiwa na ukosefu wa vifaa ndani ya hayo majengo.

“Ifikapo tar 28 jumatano mjitokeze kwa wingi kupiga kura ili kuhakikisha tunakiweka chama madarakani kutimiza ahadi tulizoziahidi.” Alisema Delphina

Hata hivyo hakusita na kutokuwa mchoyo wa fadhila Kwa mwanamke mwenzake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Kwa kazi nzuri alizozifanya kwenye Sekta ya Afya katika Serikali ya awamu ya 5, hivyo nichagueni na mimi nitakua kama Ummy.

Pia Mwl Delphina alisema kama watapata ridhaa ya kuongoza katika Jimbo la Singida kaskazini ndani ya miaka hiyo 5 watahakikisha wanasimamia vyema masuala yote yanayowahusu wafugaji na wakulima, kutunga na kutengeneza sera bora ili kuwa na ufugaji wenye tija na kilimo kwa ujumla.

“Hakika nawaambia wananchi wangu chagueni chama cha wananchi ili kiende kushirikiana na wataalamu wa kilimo, Maafisa mifugo tufuge na tulime kisasa ili tuondokane na umaskini tulionao,sasa tar 28 msifanye makosa kwa mgombea urai wetu Prof Ibrahim Lipumba mimi na Diwani wetu.” Alisema Delphina

Akifunga mkutano huo wa kampeni Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya Shabani Jumanne, aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kusikiliza sera za mgombea Ubunge,na anaamini wamemuelewa na tar 28 watakwenda kufanya maamuzi ya haki kukipatia kura chama chicho.

"Nimefurahi sana tumefanya mkutano wetu kwa amani ila napenda kuwaambia tusifanye siasa za mazoea twendeni tukafanye mabadiliko sasa tumetawaliwa kwa muda mrefu sana bila maendeleo yeyote, hebu tazameni hatuna umeme, maji safi na salama, barabara mbovu chagueni chama cha wananchi CUF kikaisimamie Serikali na kuhakikisha maendeleo haya yanapatikana katika Jimbo letu." alisema Jumanne.

No comments:

Powered by Blogger.