LIVE STREAM ADS

Header Ads

Vyuo vyalalamikiwa "havitambui vyama vya wafanyakazi"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), kimesikitishwa na mtazamo hasi wa baadhi ya wamiliki wa vyuo binafsi na umma kutokuwa tayari wafanyakazi wake kujiunga na vyama vya wafanyakazi.

Hayo yameelezwa kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu Maalum wa THTU unaofanyika jijini Mwanza kwa siku mbili kuanzia Ijumaa Septemba 04, 2020 ambao pamoja na mambo mengine una lengo la kujadili na kupitisha rasmi ya mabadiliko ya Katiba ya chama hicho.

Akifungua mkutano huo, Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alisema hakuna namna waajiri wanaweza kuzuia uwepo wa vyama vya wafanyakazi na kuahidi kufuatilia taasisi za elimu mkoani Mwanza ambazo haziko tayari kuruhusu wafanyakazi wake kujiunga na vyama vyao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) unaofanyika jijini Mwanza kwa siku mbili kuanzia Ijumaa Septemba 04, 2020.
Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), Dkt. Paul Loisulie akieleza changamoto za baadhi ya vyuo vikuu nchini kukataa kujiunga na vyama vya wafanyakazi wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), Elia Kasalile akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkuano huo.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.