LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waliogombea kurudi kazini bila masharti

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza amesisitiza kuwa watumishi wote wakiwemo waalimu walioshiriki kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu 2020 wanapaswa kurejea kazini wakiwa na stahiki zao zote kama alivyoagiza Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Mongella ameyasema hayo Septemba 03, 2020 wakati akifungua semina ya waalimu kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Kigoma, Kagera na Geita.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akifungua semina hiyo.
Semina hiyo ya siku mbili kuanzia Septemba 03, 2020 inafanyika jijini Mwanza.
Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT), Mwl. Leah Ulaya amesema waalimu wataendelea kuwa wamoja na kuliunganisha Taifa hususani wakati huu wa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu 2020.
Makamu wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mwl. Dinah Mathamani alimpongeza Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kwa namna anavyoshirikiana vyema na waalimu na kubainisha kwamba waalimu wataendelea kuyasema mazuri yanayofanywa na Serikali.
Waalimu kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa semina hiyo.
Waalimu walioshiriki semina hiyo wakifuatilia ufunguzi wake.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.