LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Bunda afungua Kongamano la Wajasiriamali

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya Bunda mkoani Mara, Mwl. Lydia Bupilipili amefungua Kongamano la Wajasiriamali wilyani humo lenye lengo la kutoa elimu kuhusu mikopo inayotolewa na Halmashauri pamoja na umuhimu wa wananchi kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu 2020.

Akifungua kongamano hilo lililowashirikisha zaidi ya wananchi elfu moja kutoka Halmashauri za Bunda Vijijini na Bunda Mji, DC Bupilipili amesema vikundi 223 vya wanawake, vijana na walemavu vimenufaika na mikopo katika kipindi cha mwaka 2015/2020.

Ameongeza kuwa fedha zilizotolewa kwenye vikundi hivyo kutoka Halmashauri za Bunda Mji na Bunda Vijijini ni shilingi Milioni 635 na hivyo kusaidia wananchi kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali za uzalishaji mali.

Katika hatua nyingine DC Bupilipili amewahimiza wananchi kutumia vyema haki yao ya msingi ya kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu 2020 kuanzia mchakato wa kampeni hadi kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaostahili kwa ajili ya maendeleo yao.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wamekiri kuwa mikopo inayotolewa na Halmashauri imekuwa na manufaa na kuomba kiwango cha fedha kinachotolewa kiongezeke ili kukidhi mahitaji. Wameomba pia changamoto ya vikundi vingine kupata mikopo kwa kujirudia huku vingine vikikosa licha ya kukidhi vigezo ishughulikiwe.

Akitoa salamu kwenye kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI, Yassin Ally ametoa rai kwa mamlaka husika kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wananchi hususani wanawake ili kushiriki bila hofu kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2020 kuanzia kampeni hadi kwenye kupiga kura.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
                Mkuu wa Wilaya Bunda mkoani Mara, Mwl. Lydia Bupilipili akifungua kongamano hlo.


No comments:

Powered by Blogger.