Kivuko kipya cha MV Ukara II chakamilika “chaingizwa majini”
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Kivuko hicho kitakachokuwa kinafanya safari zake katika visiwa vya Bugorola na Ukara wilayani Ukerewe kimeshushwa katika maji ya Ziwa Victoria Jumatatu Oktoba 12, 2020 huku wananchi na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella wakishuhudia zoezi hilo.
Rais Magufuli alitoa ahadi ya ujenzi wa kivuko hicho baada ya ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kuzama Septemba 20, 2018 kikitokea Bugorola kuelekea Ukara na kusababisha vifo kwa abiria 227 huku wengi wakiokolewa.
Mwonekano wa Kivuko kipya cha MV. Ukara II kikiingizwa majini ambapo kinatarajiwa kuanza kazi Oktoba 19, 2020 katika visiwa vya Bugorola-Ukara baada ya kufanyiwa ukaguzi.
Kivuko cha MV. Ukara II kikiingizwa majini/ ziwani.
Viongozi mbalimbali waliojitokeza kushuhudia Kivuko cha MV. Ukara kikiingizwa majini.
Kivuko cha MV. Ukara II baada ya kuingizwa majini/ ziwa Victoria.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini
No comments: