LIVE STREAM ADS

Header Ads

Zaidi ya Bilioni 70 kujenga maghala ya kisasa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Joctan Agustino, Njombe
Serikali imesema imeanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi Maghala na Maabara za kisasa za kufanya utafiti wa virutubisho utakaosaidia kukabiliana na tatizo la sumukuvu nchini utakaoghalimu shilingi bilioni 78 hadi kukamilika kwake.

Mbali na kutenga kiasi hicho kwa ajili ya ujenzi wa maghala na maabara, pia mwezi May 2020 Serikali imetenga na kuukabidhi wakala wa chakula nchini NFRA kiasi cha zaidi ya bil 47 kwa ajili ya ununuzi wa nafaka yakiwemo mahindi, mtama, uwele, mpunga na ulezi ambayo yanazalishwa kwa wingi mkoani Njombe na kutoa muongozo wa bei isiwe chini shilingi 500.

Akizungumza wakazi wa uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya siku ya chakula ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Njombe naibu waziri wa kilimo Omary Mgumba amesema Serikali imefanya jitihada kubwa katika kipindi cha muda mfupi ili kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo na hifadhi kubwa ya chakula.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi Marwa Rubirya akieleza hali ya udumavu amesema Licha ya mkoa huo kuwa kinara wa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara lakini unaongoza kitaifa kwa udumavu nchini kwa asilimia 53.6 na kwamba jitihada za kutoa elimu zimeanza huku lengo likiwa ifikapo 2022 kuwa asilimia 36 ya udumavu.

Nao wananchi wakaeleza kwamba wataitumia vyema fursa ya maonesho hayo ili kujifunza matumizi bora ya pembejeo na viuatilifu pamoja elimu ya matumizi bora ya lishe ili kuepukana na udumavu.
Kauli mbiu -Kesho Njema inajengwa na Lishe Bora Endelevu

No comments:

Powered by Blogger.