LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wasichana wilayani Ilemela wapatiwa mafunzo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Oktoa 11 kila mwaka wadau mbalimbali duniani huungana pamoja kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike, lengo likiwa ni kupaza sauti kuhakikisha jamii inatoa haki sawa baina ya mtoto wa kike na wa kiume ili wote watimize ndoto zao.

Siku hii pia inatumika kuelimisha jamii ili kupinga aina zote za vitendo vya ukatili kwa mtoto wa kike kama vile kumnyima haki yake ya kupata elimu ama kumuozesha katika umri mdogo. 

Nchini Tanzania, miongoni mwa wadau waliodhamisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani mwaka huu 2020 ni pamoja na shirika la Sauti ya Wanawake linalotekeleza mradi wa Imarisha Wasichana kwa kushirikiana na lile la MIBOS kupitia ufadhili wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto lenye makao yake makuu nchini Uganda.

Mkurugenzi wa shirika la Sauti ya Wanawake, Sophia Donald alisema tayari mabinti zaidi ya 100 walio shuleni na walio nje ya shule katika Wilaya Ilemela wapatiwa mafunzi ya ujasiriamali na afya ya uzazi kupitia mradi wa Imarisha Wasichana ambapo matarajio ni kufikia zaidi ya wasichana elfu tatu mwaka 2021 ambapo wasichana hao watakuwa chachu ya mabadiliko kwa wasichana wenzao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa Shirika la Sauti ya Wanawake, Sophia Donald akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike 2020 yaliyofanyika ukumbi wa Montesori wilayani Ilemela.
Mkurugenzi wa Shirika la Sauti ya Wanawake, Sophia Donald alisema kupitia mradi wa Imarisha Wasichana, shirika lake limewajengea uwezo zaidi ya wasichana 100 ili kujitambua ambapo hadi kufikia mwaka 2021 wanatarajia kuwafikia wasichana 3000 ambao watakuwa chachu ya mabadiliko kwa wenzao.
Mkurugenzi wa taasisi ya Star (Star Foundation), Stella Mutta ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo aliwahimiza mabinti kujitunza na kutojihusisha na mahusiano ya kimapenzi ili kutimiza ndoto zao ikiwemo kupata elimu.
Wasichana walioshiriki maadhimisho hayo wakimsikiliza meni asmi.
Mkurugenzi wa shirika la MIBOS akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo. Shirika la MIBOS kwa kushirikiana na shirika la Sauti ya Wanawake linatekeleza mradi wa Imarisha Wasichana katika Kata sita wilayani Ilemela.
Afisa Vijana Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Lucy Matenga alisema ili wasichana watimize ndoto zao ni lazima wajiamini na kujituma kwa kila jambo wanalolifanya hususani kuzingatia masomo.
Afisa Tarafa ya Ilemela mkoani Mwanza akitoa salamu za Serikali kwenye maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi akipokea risala kutoka kwa wasichana.
Katika risala yao, wasichana waliomba kuwezesha vitendea kazi ikiwemo vyerehani pamoja na mikopo ili baada ya kuhitimu mafunzo wanayopewa na shirika la Sauti ya Wanawake wajiajiri.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.