TUGHE WATEMBELEA MAKUMBUSHO YA NYERERE
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Viongozi na wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) wametembelea makumbusho ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere yaliyopo Kijiji cha Mwitongo Wilaya Butiama mkoani Mara.
Ziara hiyo ni sehemu ya mafunzo/ Semina kwa waajiri na viongozi wa matawi wa TUGHE iliyoanza tarehe 05-09 Oktoba 2020 jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Viongozi na wanachama mbalimbali wa TUGHE wakipiga picha katika kaburi la Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililopo Mwitongo Butiama mkoani Mara.
Kwa kabila la Wazanaki, kondo la nyuma baada ya mtoto kuzaliwa lilichimbiwa katikati ya nyumba hivyo eneo hili ndipo kondo la Mwl. Nyerere na wanafamilia wengine lilichimbiwa ambapo sanamu hii inaashiria kumbukumbu hiyo.
Inaelezwa kwamba chimbuko la Mwenge wa Uhuru ni kabila la Wazanaki hivyo kila Mwenge ukifika mkoani Mara hupandishwa katika jiwe hili.
Kijiji cha Mwitongo wilayani Butiama.
Baada ya mavuno, maghala (vihenge) haya ya asili yalitumika kuhifadhia mazao.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini
SOMA>>> Habari kuhusiana na TUGHE
SOMA ZAIDI Habari zaidi kuhusiana na Nyerere
No comments: