LIVE STREAM ADS

Header Ads

CRDB yanogesha Wiki ya Huduma kwa Wateja

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani mwaka huu 2020, Benki ya CRDB imewahimiza wateja wake kufika katika matawi yake ili kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo mikopo yenye riba na masharti nafuu.

Meneja Biashara wa benki hiyo Kanda ya Ziwa, Hassanalay Japhary Katura ameyasema hayo wakati akizungumza na BMG kuhusiana na maadhimisho hayo ambayo huadhimishwa wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka.

Katura amesema benki ya CRDB nchini inatoa huduma mbalimbali ikiwemo wateja wapya kufungua akaunti kwa muda mfupi, mikopo ya fedha kwa wastaafu, watumishi, akina mama pamoja na mikopo ya zana za kilimo kwa wakulima.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wateja wa benki ya CRDB wakipata huduma katika tawi la Mwanza.
Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Hassanaly Japhary Katura (kulia) akifuatilia utoaji wa huduma kwa wateja katika tawi la benki hiyo mkoani Mwanza.
Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Hassanaly Japhary Katura (kulia) akiwasiliza wateja wa benki hiyo.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.