LIVE STREAM ADS

Header Ads

ILEMELA “mgombea aahidi kuondoa rada kwenye makazi ya wananchi”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mgombea ubunge jimbo la Ilemela mkoani Mwanza kupitia chama cha ADC, Shaban Itutu amewaomba wananchi kumchagua kuwa mbunge wao ili akatumie weledi na ushawishi alionao kuhimiza maendeleo jimboni humo. 

Itutu ambaye pia ni mgombea udiwani Kata ya Kiseke aliyasema hayo wakati akiomba kura kwa wakazi wa Kata hiyo na kubainisha kuwa akifanikiwa kuchaguliwa atahakikisha anatatua kero zinazowakabili ikiwemo kuondoa rada iliyosimikwa kwenye makazi yao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mgombea ubunge jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Shaban Itutu (kulia) akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Kata ya Kisesa jimboni humo baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020. Itutu pia anagombea nafasi ya udiwani katika Kata ya Kiseke.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.