LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la SBFIC laadhimisha Wiki ya Akiba Duniani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Shirika la SBFIC (Savings Banks Foundation for International Coorperation) tawi la Tanzania limeadhimisha Siku ya Akiba Duniani 2020 na kutumia fursa hiyo kutoa elimu ya masuala ya kifedha kwa wanafunzi mkoani Mwanza.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la SBFIC, Stephen Safe amesema shirika hilo limejizatiti kutoa elimu ya kifedha kwa wanafunzi, waalimu na wazazi ili kutambua umuhimu wa masuala mbalimbali ikiwemo utunzaji akiba kwa manufaa yao ya baadae.

Naye mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya Ilemela, Dkt. Severine Lalika alipongeza jitihada zinazofanywa na shirika la SBFIC katika kutoa elimu ya kifedha na kueleza kwamba Serikali inatambua mchango huo.

Shirika la SBFIC lenye makao makuu nchini Ujeumani lilianza kutoa elimu ya masuala ya kifedha kwa wanafunzi mkoani Mwanza mwaka 2019 kwa kushirikiana na washirika wake ikiwemo benki ya Akiba ambapo kila wiki zaidi ya wanafunzi 3000 hupata elimu hiyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt. Severine Lalika akizungumza kwenye maadhimisho ya Wiki ya Akiba Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Mwanza Baptist Kona ya Bwiru.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirila la SBFIC, Stephen Safe akizungumza kwenye maadhimisho ya Wiki ya Akiba Duniani 2020.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.