LIVE STREAM ADS

Header Ads

Msimamizi wa Uchaguzi Nyamagana amuonya mgombea ubunge CHADEMA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Kiomoni Kibamba amemuonya mgombea ubunge jimboni humo kupitia CHADEMA, John Pambalu kuacha kusambaza mitandaoni taarifa zisizo sahihi kuhusiana na uwepo wa vituo hewa vya kupigia kura. 

Kibamba ametoa onyo hilo Oktoba 23, 2020 mbele ya waandishi wa habari na kufafanua kwamba taarifa iliyosambazwa na mgombea huyo haikuwa na mantiki kwa kuwa alitumia orodha ya vituo vya kupigia kura kufanyia ulinganifu kwenye orodha ya majira ya zoezi la uboreshaji daftari la wapiga kura (daftari la awali la wapiga kura).
#BMGHabari
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Nyamagana akikanusha kwa wanahabari uwepo wa kituo hewa cha kupigia kura kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.