LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wajasiriamali Magu wakabidhiwa mamilioni ya fedha na pikipiki

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Halmashauri ya Wilaya Magu mkoani Mwanza imekabidhi mikopo ya fedha taslimu pamoja na pikipiki kwa makundi mbalimbali ikiwemo vijana, akina mama na walemavu yenye thamani ya shilingi milioni 133 katika kota ya kwanza ya mwaka huu 2020.

Akikabidhi mikopo hiyo Oktoba 23, 2020 Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kali amewataka walionufaika kuitumia vyema ili kuleta tija katika shughuli zao na kuirejesha kwa wakati ikizingatiwa kwamba haina riba ili kuwanufaisha wajasiriamali wengine.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Magu, Lutengano Mwalwiba alisema katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano makusanyo katika halmashauri hiyo yameongezeka kutoka kiwango cha chini ya bilioni 1.6 hadi kufikia bilioni 3.17 na kuingia kwenye halmashauri zinazokusanya mapato ya juu ya zaidi bilioni 3.

“Lengo ni kuongeza zaidi mapato ili kuhakikisha tunatoa huduma bora ikiwa ni pamoja na mikopo, ni kweli kabisa tumezuia mivujo mingi ya mapato na sasa hali imekuwa nzuri” aliongeza Mwalwiba.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kali akizungumza kabla ya kukabidhi mikopo hiyo kwa makundi mbalimbali ikiwemo vijana, akina mama na wenye ulemavu.
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Magu, Lutengano Mwalwima akielezea mikopo inayotolewa na halmashauri hiyo kupitia mapato ya ndani.
Wajasiriamali mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya Magu wakikabidhiwa mikopo kupitia mapato ya asilimia 10.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.