LIVE STREAM ADS

Header Ads

BUNDA WAFANYA IBADA YA SHUKURANI BAADA YA UCHAGUZI MKUU

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Baada ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kurejea madarakani katika kipindi cha pili kufuatia ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bunda mkoani Mara imeandaa ibada ya kumshukuru Mungu pamoja na wananchi.
Mkuu wa Wilaya Bunda, Mwl. Lydia Bupilipili akitoa shukurani kwa wananchi baada ya kuichagua CCM katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2002 na kueleza mikakati iliyopo kwenye Ilani ya chama hicho.
Mkuu wa Wilaya Bunda, Mwl. Lydia Bupilipili alisema Serikali itahakikisha inatekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/25 ili kuwaletea wananchi maendeleo zaidi.
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Robert Maboto akitoa shukurani kwa wananchi jimboni humo baada ya kumchagua kuwa mbunge wao.
Ibada ya kumshukuru Mungu na wananchi wilayani Bunda ilifanyika Jumapili Novemba 29, 2020 katika uwanja wa Sabasaba.
Katibu wa CCM Wilayani Bunda, Ramadhani Dallo aliwataka viongozi wote waliochaguliwa kuwatumikia vyema wananchi kama Ilani ya chama hicho inavyoelekeza.
Sheikh wa BAKWATA wilayani Bunda, Abubakary Bin Ally akitoa dua.
Viongozi wa dini wilayani Bunda wakitoa maombi.
Viongozi wilayani Bunda wakiwa kwenye maombi.
Maombi ya shukurani wilayani Bunda baada ya Uchaguzi Mkuu 2020.
Kwaya mbalimbali zikitumbuiza kwenye ibada hiyo.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.