LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ya CRDB yasaidia kufanikisha Maadhimisho ya Siku ya Magonjwa Yasiyoambukiza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Benki ya CRDB imekabidhi flana kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza ili kufanikisha kilele cha maadhimisho ya Siku ya Magonjwa Yasiyoambukiza yatakayofanyika katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, Jumamosi Novemba 14, 2020.

Meneja Biashara wa benki hiyo Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly amekabidhi flana hizo Ijumaa Novemba 13, 2020 na kuahidi kwamba CRDB itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza katika kufanikisha shughuli mbalimbali zinazoratibiwa na Ofisi hiyo.

Akipokea flana hizo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella, Katibu Tawala Mkoa Mwanza Emmanuel Tutuma aliishukuru benki ya CRDB kwa kuchangia mantenti matano pamoja na flana 350 ili kufanikisha maadhimisho hayo akiongeza kuwa benki hiyo ni miongoni mwa wadau muhimu mkoani Mwanza.

Kwa Mkoa Mwanza Maadhimisho ya Siku ya Magonjwa Yasiyoambukiza 2020 wananchi wamepata fursa ya kupima bure magonjwa mbalimbali ikiwemo Saratani, kisukari, shinikizo la damu, upimaji wa macho, meno, elimu kuhusu lishe, namna ya kuzuia magonjwa yasiyoambukiza pamoja na uchangiaji wa damu kwa hiari ambapo katika kilele chake kitatanguliwa na mazoezi ya viungo.
#BMGHabari
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Emmanuel Tutuba (wa tatu kushoto) akipokea flana kutoka kwa Meneja Biashara wa CRDB Kanda ya Ziwa, Japhari Hassanaly (wa pili kulia) kwa ajili ya kilele cha siku ya magonjwa yasiyoambukiza.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.