LIVE STREAM ADS

Header Ads

WASICHANA ELFU 48 WAPATA UFADHILI WA MASOMO KUTOKA CAMFED

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wasichana zaidi ya elfu 48 waliokuwa wanaishi kwenye mazingira magumu katika mikoa mbalimbali nchini wamenufaika na ufadhili wa masomo kutoka shirika la CAMFED kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu na hivyo kutimiza ndoto zao kielimu.

Mkurugenzi wa shirika hilo, Lydia Wilbart aliyasema hayo jijini Mwanza kwenye kilele cha mafunzo kwa wasichana walioshindwa kuhitimu elimu ya kidato cha nne kutokana na changamoto mbalimbali yaliyolenga kuwajengea uwezo ili kurejea kwenye mfumo wa elimu kupitia vyuo vya ufundi.
#BMGHabari
Mkurugenzi wa shirika la CAMFED, Lydia Wilbard akizungumza wakati wa kilele cha mafunzo ya kuwajengea uwezo wasichana walioshindwa kuhitimu kidato cha nne.
Mratibu Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa Mwanza, Denis Kashaija akihitimisha mafunzo kwa wasichana walioshindwa kuhitimu kidato cha nne yaliyoandaliwa na shirika la CAMFED.
Mafunzo hayo yalifanyika jijini Mwanza.
Picha ya pamoja baada ya mafunzo hayo yaliyofanyika Gandhi Hall jijini Mwanza.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.