LIVE STREAM ADS

Header Ads

Hatuna ugomvi, tofauti ni za kawaida, tunazimaliza- Meneja NHIF

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa Mwanza, Jarlath Mushashu amesema hakuna ugomvi baina ya mfuko huo na watoa huduma za afya mkoani Mwanza na kwamba changamoto zinapojitokeza hukaa pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.

Mushashu ameyasema wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za NHIF mkoani Mwanza kwenye kikao kazi baina ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Benard Konga na watoa huduma za afya kilichofanyika Disemba 23, 2020 ukumbi wa BOT jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Watoa huduma zaidi ya 300 wameshiriki kikao hicho.
Kikao hicho kimelenga kujadili masuala mbalimbali ikiwemo malipo makato ya watoa huduma za afya baada ya kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.