LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella asisitiza maadili na uadilifu “Magufuli atapumzika”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amewataka watumisha wa umma na binafsi kuzingatia maadili na uadilifu katika utendaji wao wa kazi wakifuata nyayo za Rais Dkt. John Pombe Magufuli hatua itakayosaidia taifa kusonga mbele zaidi kimaendeleo. 

Mongella alitoa rai hiyo Disemba 10, 2020 wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani yaliyoambatana na kongamano la elimu kwa viongozi na watumishi mbalimbali wa Serikali. 

Alisema kila mtumishi akiamua kuwa mwadilifu kama Rais Dkt. Maguguli maendeleo yatakwenda kwa kasi. “mtu mmoja tu kaja mmeona maendeleo yalivyokwenda kwa kasi ndani ya miaka mitano, je katika watu milioni 60 wakatokea hata watu 100 tu nchi yetu itakwenda wapi?” alihoji Mongella. 

Naye Katibu Msaidizi wa Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Ziwa, Godson Kweka alisema dhana ya maadili, uadilifu, uwazi na uwajibikaji huchochea utawala bora hivyo viongozi wanapaswa kuzingatia sheria ya maadili kwani inatoa mwongozo wa jinsi ya kuenenda.

Taarifa iliyotolewa na TAKUKURU mkoani Mwanza kwenye maadhimisho hayo katika kipindi cha mwaka 2019/20, idara ya Serikali za Mitaa iliongoza kwa kulalamikiwa na wananchi kwa kuminya ama kuchelewesha utoaji haki ikifuatiwa na idara ya elimu, mahakama, taasisi za fedha pamoja na polisi ambapo katika taarifa hiyo taasisi za dini nazo zimelalamikiwa pia.
#BMGHabari
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Disemba 10, 2020. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Emmanuel Tutuba.
Katibu Msaidizi wa Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Ziwa, Godson Kweka alisema maadili hutoa mwenendo mwema, haki, usawa kwa makundi mbalimbali katika jamii pamoja na watumishi wa umma na huchochea utawala bora na wa sheria.
Viongzi mbalimbali mkoani Mwanza wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.