Utapeli mpya waibuka vyuoni “wanafunzi wa kike wako hatarini zaidi”
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wimbi la wanafunzi hususani wa kike katika vyuo mbalimbali nchini kunasa kwenye matapeli wa mahusiano ya kimapenzi limeelezwa kuchochea ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kutelekezwa baada ya kupata ujauzito na hivyo kuathiri masomo yao.
Hayo yamebainika Disemba 12, 2020 kwenye kongamano la utoaji elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa chuo cha teknolojia Dar es salaam (DIT) kampasi ya Mwanza, lililoandaliwa na uongozi wa chuo hicho kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.
Wanafunzi wa chuo cha DIT Mwanza wakifuatilia kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally alitoa rai kwa wanafunzi vyuoni kujiepusha na muweweseko wa pete tegesha za uchumba ili wakaposti mtandaoni kwani zinawakwamisha kimasomo.
Baadhi ya wanafunzi wa DIT kampasi ya Mwanza walikiri kuwa matapeli wa mapenzi vyuo wanasababisha wanafunzi wengi kushindwa kutimiza ndoto zao.
Waziri Mkuu Serikali ya wanafunzi DIT kampasi ya Mwanza, Hamis Bakari akieleza namna vitendo vya mapenzi vinavyoathiri masomo kwa wanafunzi hususani wa kike vyuoni.
Wanafunzi wa DIT Mwanza wakiwa kwenye kongamano hilo.
Wanafunzi wa DIT Mwanza wakifuatilia mada kwenye kongamano hilo.
Mmoja wa wanafunzi akichangia mada kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea...
Wanahabari wakinasa matukio kwenye kongamano hilo.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Chuo cha DIT kampasi ya Mwanza, Dkt. Albert Mmari (wa tatu).
Viongozi mbalimbali meza kuu wakifuatilia kongamano hilo.
Mkuu wa Chuo cha DIT kampasi ya Mwanza, Dkt. Albert Mmari (kushoto) alisema chuo hicho imeanzisha kamati ya jinsia kwa ajili ya kushughulikia masuala mbalimbali ya kijinsia ikiwemo kuelimisha na kuhamasisha wanafunzi kujitambua na kutimiza malengo yao wawapo chuoni.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kongamanp hilo.
Wanafunzi chuo cha DIT Mwanza wakifuatilia kongamano hilo.
Mmoja wa wanafunzi akifurahia jambo.
Kongamano hilo lililenga kuwajengea uwezo wanafunzi kujitambua na kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia vyuoni.
Kongamano hilo lilifanyika viunga vya DIT kampasi ya Mwanza wilayani Ilemela.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: