LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Waziri OR-TAMISEMI atoa siku 60 kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Festo John Dugange ametoa muda wa miezi miwili kwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri kuweka mikakati ya kupata vita tiba kwa ajili ya majengo mapya ya Vituo vya Afya na Hospitali. 

Dkt. Dugange ametoa agizo hilo Disemba 14, 2020 baada ya kukagua ujenzi wa jengo la wazazi katika Zahanati ya Fumagila Kata ya Kishiri jijini Mwanza, uliogharimu shilingi milioni 137 kati ya shilingi milioni 200 zilizotolewa na Serikali ambapo chechi iliyobaki imeanza kutumika kwenye ujenzi wa jengo la maabara katika Zahanati hiyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Festo John Dugange akizungumzia lengo la ziara yake alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akitoa taarifa ya maendeleo baada ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Festo John Dugange kufika ofisini kwake kabla ya kuanza ziara ya kutembelea miradi ya afya.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akitoa salamu zake.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Costantine Sima akitoa salamu zake.
Kutoka kulia Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Festo John Dugange, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula na Mstahiki Meya Jiji la Mwanza Costantine Sima.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Festo John Dugange alikagua ujenzi wa jengo la wazazi katika Zahanati ya Fumagila jijini Mwanza.
Ujenzi wa jengo la maabara katika Zahanati ya Fumagila jijini Mwanza.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Festo John Dugange akishiriki ujenzi wa jengo la maabara katika Zahanati ya Fumagila jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.