BENKI YA CRDB YAKABIDHI MADAWATI, MEZA NA VITI KUBORESHA ELIMU MSALALA, USHETU - SHINYANGA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Rose Robert Manumba (kulia) viti na meza kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ikinda iliyopo kwenye Kata ya Ikinda Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB katika shule ya Msingi Ngilimba iliyopo Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana akimkabidhi Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Gloria Absalum (kulia) Madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB katika shule ya Msingi Ngilimba iliyopo kwenye kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Rose Robert Manumba (kulia) viti na meza kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ikinda iliyopo kwenye Kata ya Ikinda Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.
# Shule ya Msingi Ngilimba na Sekondari Ikinda zanufaika
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB imekabidhi jumla ya viti 40 na meza 40 kwa Shule ya Sekondari Ikinda iliyopo Kata ya Ikinda, Halmashauri ya Msalala, pamoja na madawati 40 kwa Shule ya Msingi Ngilimba iliyopo Kata ya Ulowa, Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kielimu wa “Keti Jifunze”.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Septemba 17, 2025, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana, amesema lengo la benki hiyo ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki na yenye hamasa ya kujifunza.
“Meza, viti na madawati haya ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kupitia mradi wa Keti Jifunze, unaolenga kupunguza changamoto ya uhaba wa miundombinu shuleni na kuongeza usawa wa elimu kati ya mijini na vijijini,” amesema Wagana.
Ameongeza kuwa CRDB haitoi huduma za kifedha pekee bali pia inagusa maisha ya jamii kwa kushirikiana na serikali kutatua changamoto za sekta ya elimu, ili kila mtoto apate fursa ya kusoma katika mazingira bora.
Akizungumza wakati wa kupokea madawati kwa niaba ya Shule ya Msingi Ngilimba, Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Gloria Absalum, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda ameishukuru CRDB kwa msaada huo na kuahidi kuyatunza madawati hayo.
Sehemu ya madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB katika shule ya Msingi Ngilimba iliyopo Halmashauri ya Ushetu.
Amefafanua kuwa Halmashauri ya Ushetu imetenga zaidi ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya ukamilishaji wa darasa moja, huku akiwataka wazazi na wadau kushirikiana na serikali kuboresha zaidi miundombinu ya shule.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Rose Robert Manumba, amepokea meza na viti kwa niaba ya Shule ya Sekondari Ikinda na kuipongeza CRDB kwa kushirikiana na serikali kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu.
“Serikali ya Awamu ya Sita imefanya kazi kubwa ya kujenga madarasa na kuboresha shule. Ushirikiano wa wadau kama CRDB unasaidia kasi hii ya maendeleo,” amesema Manumba.

Sehemu ya viti na meza zilizotolewa na Benki ya CRDB katika shule ya Sekondari Ikinda Halmashauri ya Msalala.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ngilimba, Erick Issangya, amesema shule hiyo yenye wanafunzi 550 sasa inakuwa na madawati 100, ingawa bado inahitaji zaidi ya madawati 83 pamoja na nyumba za walimu na umeme.
Kwa upande wake, Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Msalala, Elias Nyabenda, amesema Shule ya Sekondari Ikinda yenye wanafunzi 223 sasa imepata nyenzo zitakazowasaidia kujifunza vizuri zaidi.
Wanafunzi walionufaika na msaada huo akiwemo Annastazia Gabriel wa Shule ya Msingi Ngilimba na Rasta Petro wa Shule ya Sekondari Ikinda wameonesha furaha yao huku wakiishukuru CRDB kwa msaada huo na kuomba msaada zaidi katika nyanja zingine.
Benki ya CRDB imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuwekeza katika elimu kupitia mradi wake wa kitaifa wa “Keti Jifunze”, unaolenga kuboresha mazingira ya ujifunzaji kwa watoto wa Kitanzania kote nchini.
Mradi huu, ambao ni sehemu ya mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii wa benki hiyo, umejikita katika kupunguza changamoto kubwa zinazozikabili shule za umma, ikiwemo uhaba wa madawati, meza, viti, madarasa na vyoo.
Kupitia hatua hizo, CRDB inasaidia kuongeza usawa wa elimu kati ya mijini na vijijini na kuweka mazingira bora zaidi ya kujifunzia kwa wanafunzi.
Tangu uzinduliwe, Keti Jifunze umefika katika shule nyingi nchini, ukigusa maelfu ya wanafunzi. Kupitia mpango huu, CRDB imetoa madawati ,meza , viti na vifaa vingine vya shule, na hivyo kuchangia pakubwa katika kufanikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa elimu bora na jumuishi.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana akizungumza Septemba 17,2025 wakati CRDB ikikabidhi viti na meza katika shule ya Sekondari Ikinda iliyopo kwenye Kata ya Ikinda Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Rose Robert Manumba. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana akizungumza Septemba 17,2025 wakati CRDB ikikabidhi viti na meza katika shule ya Sekondari Ikinda iliyopo kwenye Kata ya Ikinda Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Rose Robert Manumba akizungumza Septemba 17,2025 wakati CRDB ikikabidhi viti na meza katika shule ya Sekondari Ikinda iliyopo kwenye Kata ya Ikinda Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Rose Robert Manumba akizungumza wakati CRDB ikikabidhi viti na meza katika shule ya Sekondari Ikinda iliyopo kwenye Kata ya Ikinda Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana akiandika dondoo muhimu wakati CRDB ikikabidhi viti na meza katika shule ya Sekondari Ikinda iliyopo kwenye Kata ya Ikinda Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Rose Robert Manumba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Rose Robert Manumba akiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya meza na viti kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ikinda.
Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Msalala, Elias Nyabenda akisoma taarifa kuhusu shule ya Sekondari Ikinda.
Muonekano wa sehemu ya viti na meza zilizotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ikinda iliyopo kwenye Kata ya Ikinda Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Rose Robert Manumba (kulia) viti na meza kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ikinda iliyopo kwenye Kata ya Ikinda Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.
Makabidhiano ya viti na meza kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ikinda iliyopo kwenye Kata ya Ikinda Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.
Mwanafunzi Rasta Petro wakati Shule ya Sekondari Ikinda akitoa neno la shukrani kwa Benki ya CRDB na Serikali kufanikisha upatikanaji wa viti na meza katika shule hiyo.
Picha za kumbukumbu wakati Benki ya CRDB ikikabidhi viti na meza kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ikinda iliyopo kwenye Kata ya Ikinda Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.

Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ikinda iliyopo kwenye Kata ya Ikinda Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.
Picha ya kumbukumbu wafanyakazi wa Benki ya CRDB

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana na Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Gloria Absalum (kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda) wakikata utepe wakati makabidhiano ya Madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB katika shule ya Msingi Ngilimba iliyopo kwenye kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana (kushoto) na Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Gloria Absalum (kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda) wakikata utepe wakati makabidhiano ya Madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB katika shule ya Msingi Ngilimba iliyopo kwenye kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Gloria Absalum (kulia) akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ngilimba, Erick Issangya ,Madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB katika shule ya Msingi Ngilimba iliyopo kwenye kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga.
Viongozi na wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye Madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB katika shule ya Msingi Ngilimba iliyopo kwenye kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga.
Viongozi na wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye Madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB katika shule ya Msingi Ngilimba iliyopo kwenye kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Gloria Absalum akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda wakati Benki ya CRDB ikikabidhi madawati katika shule ya Msingi Ngilimba.
Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Gloria Absalum akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda wakati Benki ya CRDB ikikabidhi madawati katika shule ya Msingi Ngilimba.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Msingi Ngilimba Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga.

Muonekano wa sehemu ya madawati na wanafunzi katika shule ya Msingi Ngilimba iliyopo Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya madawati na wanafunzi katika shule ya Msingi Ngilimba iliyopo Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ngilimba, Erick Issangya akisoma taarifa ya shule wakati Benki ya CRDB ikikabidhi madawati katika shule ya Msingi Ngilimba iliyopo Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga.
Mwanafunzi Annastazia Gabriel akitoa neno la shukrani wakati Benki ya CRDB ikikabidhi madawati katika shule ya Msingi Ngilimba iliyopo Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga.
Sehemu ya wazazi na wanafunzi wakifuatilia hafla ya makabidhiano ya madawati.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments: