MARIAM IBRAHIM AWAOMBA WANANCHI WA BAGAMOYO KUMPIGIA KURA MGOMBEA URAIS DK. SAMIA
Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mariam Ibrahim, amewataka wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kumpigia kura Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea wengine wa chama hicho.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika wilayani humo jana Septemba 17, 2025, Mariam alipiga magoti mbele ya wananchi akisisitiza mshikamano na mshikikano wa kisiasa kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Mariam alisema ni muhimu Rais Samia, Mgombea Ubunge wa Bagamoyo Subira Mgalu, na madiwani wa CCM katika kata mbalimbali wakapewa kura nyingi ili kuendeleza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.
Aidha, aliwahimiza wanawake kushirikiana kikamilifu katika kampeni na kuhamasisha jamii nzima kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi, akibainisha kuwa ushiriki wao ni nyenzo muhimu ya kuendeleza maendeleo ya Bagamoyo na taifa kwa ujumla.
No comments: